AJUZA AZUA GUMZO
Wednesday, November 2, 2016
November 9 2015 ikiwa ni siku nne baada Rais Magufuli kuapishwa alifanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kukutana na changamoto kadhaa ambapo alitoa maagizo kwa Uongozi wa Hospitali kwamba, mashine ya Magnetic Resonance Imaging (MRI) na Computerized Tomography Scan (CT-Scan) ambazo zilikuwa zimeharibika ziwe zinafanya kazi katika kipindi cha siku 14.
Maagizo mengine ni pamoja na wagonjwa waliolala chini wawe wamepata vitanda pamoja na wagonjwa wote kupata dawa kupitia maduka ya dawa yaliyopo Hospitalini hapa. Na kuagiza Bohari Kuu ya Dawa (Medical Stores Department–MSD), kufungua duka la dawa ndani ya Hospitali ili kuondoa ukosekanaji wa dawa ambao ulikuwa unasababisha wagonjwa walazimike kununua dawa katika maduka binafsi yaliyopo nje ya Hospitali.
Leo November 1 2016, ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu Rais Magufuli atoe maagizo hayo, mkuu wa kitengo cha mawasiliano ya umma Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Bubwerwa Aligaesha wakati akizungumzia mafanikio ya mwaka mmoja ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Magufuli amebainisha utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli
>>>’Matengenezo ya mashine ya MRI yalifanyika kikamilifu na hadi hivi sasa mashine hii inaendelea kufanya kazi vizuri ambapo kwa kipindi cha December 2015 hadi October 25, 2016 wagonjwa 17,951 wamepimwa ukilinganisha na wagonjwa 1,911waliopima December 2014 hadi October 2015′;-Aminiel Bubwerwa Aligaesha
>>>’Mashini ya CT-Scan ilitengenezwa kikamilifu na hadi hivi sasa mashine hii inaendelea kufanya kazi vizuri ambapo kwa kipindi cha December 2015 hadi October 2016 wagonjwa 10,259 wamepimwa ukilinganisha na wagonjwa 3,319 waliopimwa December 2014 hadi October 2015′;- Aminiel Bubwerwa Aligaesha
Vyuo vikuu 15 Tz vyatakiwa kuwasilisha matokeo ya mitihani yake
Serikali imetoa siku mbli kwa vyuo vikuu 15, kuwasilisha matokeo ya mitihani kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ya wanafunzi wanaonufaika na mikopo wanaoendelea na masomo ili kupangiwa mikopo kwa mwaka wa 2016/2017.
Vyuo hivyo vilivyokuwa viwasilishe matokeo hayo siku 30 kabla ya kufunguliwa, vimepewa siku hizo kuanzia Jumanne hii, kabla serikali haijachukua hatua zozote. Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Maimuna Tarishi alisema hayo Jumanne hii, alipotembelea ofisi za Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa elimu ya juu.
Tarishi alisema baadhi ya vyuo vimeshindwa kuwasilisha matokeo ya mitihani kwa wanafunzi wanaoendelea ili wapangiwe mikopo kwa mwaka unaoendelea, kwani utaratibu lazima vyuo kuwasilisha matokeo kuonesha wanafunzi wangapi wana sifa za kuendelea kupewa mikopo.
“Bodi ya mikopo ipo katika hatua ya mwisho za utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu lakini katika utekelezaji huo tumepata changamoto kwa baadhi ya vyuo na vyuo hivyo viko jumla yao 15 ambavyo havijaleta matokeo ya mitihani kwa wale wanafunzi wanao endelea kwahiyo bodi inashindwa kuendelea na malipo,”alisema Tarishi.
Tarishi alivitaja vyuo ambavyo havijawasilisha matokeo hayo kuwa ni Vyuo vya Elimu ya Biashara (CBE) Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma, Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UOB), Chuo Kikuu cha St. John Kituo cha St Mark Dar es Salaam (SJUTDSM), Chuo cha St. John Tanzania (SJUT) na Chuo Kikuu cha Tumaini Mbeya (TUMAMBEYA).
Vingine ni Chuo cha Maendeleo ya Jamii (CDTI), Chuo cha United African University of Tanzania (UAUT), Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), Chuo Kikuu Cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph cha Tiba ya Sayansi (STJCAHS), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Kituo cha Makambako na Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU).
Serikali ya awamu ya tano imesema imejipanga kikamilifu na imetenga fedha za kutosha na tayari imetoa shilingi bilioni 80.89 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi, wanaonufaika na mikopo hiyo kwa robo ya kwanza ya mwaka.
DIAMOND PLATNUMZ maarufu kama "Chibu Dangote" |
Mwanamuziki nguli wa kizazi kipya Diamond Platnumz mapema wiki hii ameamsha hisia za mashabiki wake kwa kuposti mjengo wake mpya ambao upo SA [South Africa]. Diamond ambaye anasifa kwa muziki wake nje na ndani ya nchi na kwa kukubalika na rika zote ameposti mjengo wake huo wenye thamani ya shilingi za kitanzania si chini ya milioni mia tatu, jambo ambalo lilizua maneno mengi miongoni mwa mashabiki wake na wasio mashabiki wake.
DIAMOND PLATNUMZ AKIONESHA BAADHI YA MAENEO YA NYUMBA YAKE. |
RAIS JOHN P. MAGUFULI |
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr JOHN P. MAGUFULI mapema wiki hii ameadhimisha miaka kadhaa tangu kuzaliwa kwake. Rais huyo ambaye ameingia serikalini kwa kasi mwishoni mwa mwaka jana ameshukuru vyombo vya habari kwa ushirikiano wanaouonesha katika kipindi hiki ambacho yupo serikalini pia amewashukuru wote ambao wamemtakia heri yake ya kuzaliwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)